NBS Yajipanga Kuanzisha Kliniki Tembezi ya Takwimu, SG Apongeza e-Utendaji
Ofisi ya Taifa ya Takwimu - NBS imejipanga kuanzisha Kiliniki Tembezi ya Takwimu ili kuhakikisha Takwimu zinazozalishwa na Ofisi hiyo zinawafikia wahusika na zinatumika ipasavyo katika mipango mbalimbali ya maendeleo badala ya takwimu hizo kubaki makabatini. Kauli hiyo imetolewa na Mtakwimu Mkuu wa Serikali - SG, Dkt. Amina Msengwa alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja ya kuwajengea uwezo Watumishi wa Ofisi hiyo kuhusu utendaji kazi katika utumishi wa umma ambayo yanaratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Ngorngoro uliopo katika Jengo la Makao Makuu ya NBS jijini Dodoma tarehe 10 Mei 2026.