Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2019 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2019. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 115.92 mwezi Septemba, 2019 kutoka 112.12 mwezi Septemba, 2018.    

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Septemba, 2019