Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020 umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2020 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2020. Fahirisi za Bei zimeongezeka hadi 120.74 mwezi Juni, 2020 kutoka 117.03 mwezi Juni, 2019.      

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Juni 2020