Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2021 umeongezeka kutoka asilimia 3.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2021 hadi asilimia 3.3.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2021 imeongezeka ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Machi, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 100.63 mwezi Aprili, 2020 hadi 103.95 mwezi Aprili, 2021.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Aprili, 2021