Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi. Jedwali Namba 1 hapo juu linaonesha kuwa, Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2021 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.2 kutoka asilimia 4.1 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2021. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2021 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2021. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 100.73 mwezi Desemba, 2020 hadi 104.92 mwezi Desemba, 2021.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Desemba,2021