Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022 umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.5 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Juni, 2022. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2022 imeongezeka kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi June, 2022. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 104.32 mwezi Julai, 2021 hadi 109.05 mwezi Julai, 2022.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Julai,2022.