Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2023 umefika asilimia 4.0 kutoka asilimia 4.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2023.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Mei, 2023 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Aprili, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 108.42 mwezi Mei, 2022 hadi 112.72 mwezi Mei, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Mei,2023.