Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi kwa Tanzania Bara wa Mwaka 2017-18 ulifanywa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ikishirikiana na Idara ya Kuondoa Umaskini ya Wizara ya Fedha na Mipango. Utafiti huu ulipata fedha kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania na Wadau wa Maendeleo ambao ni pamoja na Benki ya Dunia (WB), Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Wanawake (UN Women), Ubalozi wa Ireland, Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Watoto (UNICEF) na Shirika la Msaada la Canada (GAC). Msaada wa kitaalam ulitolewa na WB, UN Women na UNICEF.

Utafiti wa HBS 2017-18 unaonesha kuwa wastani wa matumizi ya kaya moja kwa mwezi kwa Tanzania Bara ni shilingi 416,927. Kiwango hiki cha matumizi ni kikubwa kwa Maeneo ya Mijini (TZS 534,619) kuliko Maeneo ya Vijijini (TZS 361,956).

Umaskini wa mahitaji ya msingi umepungua kutoka asilimia 28.2 mwaka 2011-12 hadi asilimia 26.4 mwaka 2017-18. Vile vile, kiwango cha umaskini wa chakula kimepungua kutoka asilimia 9.7 mwaka 2011-12 hadi asilimia 8.0 mwaka 2017-18

Bonyeza hapa kusoma Chapisho la Matokeo ya Viashiria Muhimu

Bonyeza hapa kusoma Chapisho la Matokeo ya Viashiria Muhimu