Kwa mujibu wa takwimu mpya za mwaka wa kizio wa 2015, Pato halisi la Taifa lilikua kwa asilimia 7.0 mwaka 2018 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 mwaka 2017.

Ukuaji huu ulichochewa zaidi na kuongezeka kwa uwekezaji hususan katika miundombinu kama vile ujenzi wa barabara, reli, na viwanja vya ndege; kutengemaa kwa upatikanaji wa nishati ya umeme; kuimarika kwa huduma za usafirishaji; na hali nzuri ya hewa kwa ajili ya kilimo.Sekta zilizokuwa na viwango vikubwa vya ukuaji ni pamoja na: sanaa na burudani iliyokua kwa asilimia 13.7; ujenzi (asilimia 12.9); uchukuzi na uhifadhi mizigo (asilimia 11.8); na habari na mawasiliano (asilimia 9.1).

Bonyeza HAPA kusoma Kitabu chenye taarifa kamili ya Hali ya Uchumi kwa mwaka 2018 (Pdf file 3MB)

Pakua Kitabu hiki cha Hali ya Uchumi kwa mwaka 2018 (Zip file 2.4MB)