Tanzania Bara kupitia Ofisi ya Takwimu ya Taifa (NBS) ilifanya utafiti kwa mara ya kwanza mwaka 2021/22 kuhusu athari ya upatikanaji wa nishati endelevu. Utafiti huu ulifadhiliwa kwa pamoja chini ya Serikali ya Tanzania na Wakala wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Norway (Norad) kupitia Ofisi ya Takwimu ya Norway (SSB).

Taasisi zote kuu za sekta ya nishati Tanzania Bara zilishiriki katika Utafiti wa Athari ya Upatikanaji wa Nishati Endelevu (IASES) 2021/22, ambazo ni Wizara ya Nishati, Kampuni ya Utoaji Umeme Tanzania (TANESCO), Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA)

Matokeo ya utafiti wa IASES ya mwaka 2021/22 yatatumiwa kufuatilia Maendeleo Endelevu ya Dunia kwenye lengo namba 7 (SDG 7) “Kuhakikisha upatikanaji wa nishati nafuu, imara, endelevu na ya kisasa kwa wote” na Shabaha 7.1 (Kufikia mwaka 2030, kuhakikisha upatikanaji wa nishati nafuu, imara na huduma za nishati endelevu kwa wote). Pia, inatarajiwa kuwa takwimu kutoka kwenye utafiti huu itatumika katika uundaji na mapitio ya sera, kuweka mipango, na kufanya maamuzi sahihi yanayotegemea takwimu.

Bonyeza hapa kusoma Matokeo muhimu