• UZINDUZI WA MATOKEO YA UTAFITI WA MSINGI (BASELINE SURVEY) ULIOFANYIKA TANZANIA MWAKA 2018.

 

  • MWANZO WA TANZANIA KURIPOTI KIASHIRIA NAMBA 1.4.2 CHA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU

 

Utafiti huu wa msingi uliofanyika Tanzania kati ya mwezi Septemba na Novemba mwaka 2018 ni  mfululizo wa tafiti za majaribio mbili zilizofanyika nchini mwaka 2016/17 na mwanzoni mwa mwaka 2018. Lengo kuu la utafiti huu ilikuwa kupata taarifa juu ya haki na usalama katika umiliki wa ardhi na makazi na namna watu wanavyoona na kutathmini juu ya hatima ya usalama wa miliki zao kwa kuzingatia jinsia na aina ya miliki hizo.

 

Sampuli wakilishi kitaifa ya watu wenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea walihojiwa kutoka kaya binafsi nchini kujua rasilimali wanazomiliki katika makazi yao au mbali na makazi pamoja na hali ya usajili na usalama wa mali hizo. Utafiti huo ulifanyika kwa maeneo ya mjini na vijijini. Utafiti kama huu pia ulifanyika duniani kote mpaka mwaka 2018 ukihusisha jumla ya nchi 33 zikiwemo nchi tisa kutoka kanda ya kusini na mashariki mwa Afrika ikiwemo Tanzania. Kanda nyingine zilizohusika ni pamoja na Afrika ya kati na magharibi, mashariki ya kati na kaskani mwa Afrika, Latini Amerika, kusini – mashariki mwa bara la Asia na Uingereza.

Ripoti hii ilizinduliwa rasmi na Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angelina Mabula (Mb) katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Makao Makuu – Dodoma tarehe 03 Mei,2019.  

Kwa matokeo kamili ya utafiti huo bonyeza HAPA