Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2023 umebaki katika asilimia 3.3 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2023.

Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Agosti, 2023 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Julai, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 108.63 mwezi Agosti, 2022 hadi 112.25 mwezi Agosti, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Agosti,2023