Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa kipimo cha mwaka unapima kiwango cha kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2024 umebaki katika asilimia 3.0 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2023 Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Januari, 2024 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 110.81 mwezi Januari, 2023 hadi 114.09 mwezi Januari, 2024.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Januari,2024(pdf)