Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2023 umepungua hadi asilimia 3.0 kutoka asilimia 3.2 kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2023. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Desemba, 2023 imepungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 110.01 mwezi Desemba, 2022 hadi 113.34 mwezi Desemba, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Desemba,2023(pdf)