Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2023 umebaki katika asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2023. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Novemba, 2023 imebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 109.16 mwezi Novemba, 2022 hadi 112.67 mwezi Novemba, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Novemba,2023(pdf)