Mfumuko wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2023 umepungua kidogo hadi asilimia 3.2 kutoka asilimia 3.3 kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2023. Hii inamaanisha kuwa, kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia mwezi Oktoba, 2023 imepungua kidogo ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia mwezi Septemba, 2023. Fahirisi za Bei zimeongezeka kutoka 108.73 mwezi Oktoba, 2022 hadi 112.18 mwezi Oktoba, 2023.

Bonyeza hapa kupata Mfumuko wa Bei kwa mwezi Oktoba,2023